Showing posts with label MATUKIO. Show all posts
Showing posts with label MATUKIO. Show all posts

Sunday, 1 October 2017

Injini ya ndege yaharibika vibaya angani


Ndege moja kubwa ya abiria ya AirFrance, muundo wa Airbus 380, imelazimika kutua kwa dharura baada ya injini yake moja kuharibika vibaya, ndege hiyo ikiwa angani.

Ndege hiyo superjumbo ilikuwa njiani kuelekea Los Angeles- Marekani kutoka mji mkuu wa Ufaransa- Paris, ikiwa na zaidi ya abiria 500.
Iliamua kutua kwa dharura katika uwanja wa ndege wa kijeshi wa Goose Bay, mashariki mwa Canada

Bawa la ndege halikuharibika vibaya, hatua iliyosababisha ndege hiyo kutua uwanjani vyema
Hakuna mtu aliyejeruhiwa katika kisa hicho, lakini abiria walisalia ndegeni kwa saa kadhaa, baada ya ndege hiyo ya abiria kutua.
Wakati wa kisa hicho, ndege hiyo ilikuwa imewabeba abiria 496 na wafanyikazi 24. Hayo ni kwa mjibu wa msemaji wa Air France spokesperson, aliyezungumza na shirika la habari la AFP.
David Rehmar, mekanika wa zamani ambaye alikuwa abiria katika ndege hiyo, ameiambia BBC kuwa, kutokanana na uchunguzi wake, kisa hicho huenda kilitokana na kushindwa kwa feni ya injini ya ndege hiyo.

Anasema kuwa kulitokea ghafla, baada ya mlio mkubwa kusikika, ambayo ilisababisha taharuki miongoni mwa abiria

Nyumba ya Prof Jay yabomolewa na hii ndo kauli yake

Mbunge wa Mikumi kupitia CHADEMA ambaye pia ni msanii mkongwe wa bongo fleva Prof Jay, kwa Mara ya kwanza ametoa ya moyoni baada ya nyumba yake kubomolewa na TANROADS

Kwenye ukurasa wake wa instagram Prof Jay ameandika ujumbe akisema amejifunza kumshukuru Mungu, huku akuonyeshwa kushangazwa na kitendo cha serikali kutoheshimu uamuzi wa mahakama kama mhimili wa nchi.

"Sijawahi kuumia kiasi hiki, nimesikitishwa sana jinsi Tanroads wanavyoweza kujichukulia maamuzi bila ya kujali mhimili muhimu wa Mahakama wametoa maagizo gani. Na taratibu zilizotumiwa kubomoa nyumba yangu bila ya mimi na Tanesco kupewa taarifa saa kumi na mbili jioni (haukuwa muda wa kazi) na kubomoa huku umeme ukiwa unawaka ni kitendo ambacho kwanza kina hatarisha maisha ya wabomoaji wenyewe, maisha ya familia yangu pamoja na majirani zangu , limenisikitisha zaidi", ameandika Prof. Jay.

Kwa mujibu wa Prof Jay nyumba yake imebomolewa Septemba 29,2017, na hakufanikiwa kuokoa kitu chochote ambacho kilikuwemo.