Mbunge wa Mikumi kupitia CHADEMA ambaye pia ni msanii mkongwe wa bongo
fleva Prof Jay, kwa Mara ya kwanza ametoa ya moyoni baada ya nyumba yake
kubomolewa na TANROADS
Kwenye ukurasa wake wa instagram Prof Jay ameandika ujumbe akisema
amejifunza kumshukuru Mungu, huku akuonyeshwa kushangazwa na kitendo cha
serikali kutoheshimu uamuzi wa mahakama kama mhimili wa nchi.
"Sijawahi kuumia kiasi hiki, nimesikitishwa sana jinsi Tanroads
wanavyoweza kujichukulia maamuzi bila ya kujali mhimili muhimu wa
Mahakama wametoa maagizo gani. Na taratibu zilizotumiwa kubomoa nyumba
yangu bila ya mimi na Tanesco kupewa taarifa saa kumi na mbili jioni
(haukuwa muda wa kazi) na kubomoa huku umeme ukiwa unawaka ni kitendo
ambacho kwanza kina hatarisha maisha ya wabomoaji wenyewe, maisha ya
familia yangu pamoja na majirani zangu , limenisikitisha zaidi",
ameandika Prof. Jay.
Kwa mujibu wa Prof Jay nyumba yake imebomolewa Septemba 29,2017, na hakufanikiwa kuokoa kitu chochote ambacho kilikuwemo.