Sunday, 1 October 2017

Nyumba ya Prof Jay yabomolewa na hii ndo kauli yake

Mbunge wa Mikumi kupitia CHADEMA ambaye pia ni msanii mkongwe wa bongo fleva Prof Jay, kwa Mara ya kwanza ametoa ya moyoni baada ya nyumba yake kubomolewa na TANROADS

Kwenye ukurasa wake wa instagram Prof Jay ameandika ujumbe akisema amejifunza kumshukuru Mungu, huku akuonyeshwa kushangazwa na kitendo cha serikali kutoheshimu uamuzi wa mahakama kama mhimili wa nchi.

"Sijawahi kuumia kiasi hiki, nimesikitishwa sana jinsi Tanroads wanavyoweza kujichukulia maamuzi bila ya kujali mhimili muhimu wa Mahakama wametoa maagizo gani. Na taratibu zilizotumiwa kubomoa nyumba yangu bila ya mimi na Tanesco kupewa taarifa saa kumi na mbili jioni (haukuwa muda wa kazi) na kubomoa huku umeme ukiwa unawaka ni kitendo ambacho kwanza kina hatarisha maisha ya wabomoaji wenyewe, maisha ya familia yangu pamoja na majirani zangu , limenisikitisha zaidi", ameandika Prof. Jay.

Kwa mujibu wa Prof Jay nyumba yake imebomolewa Septemba 29,2017, na hakufanikiwa kuokoa kitu chochote ambacho kilikuwemo. 

No comments: